Ndugu zangu watanzania,
Kama ni kunyonywa, tumenyonywa,
Kama ni kunyanyaswa, tumenyanyaswa,
Kama ni kuonewa, tumeonewa sana,
Kama ni kuuawa mikononi mwa wa watawala wetu, tumeuawa sana,
Kama ni kucheleweshewa maendeleo, tumecheleweshwa sana,
Kama ni kuteseka, tumeteseka sana,
Kama ni kudharirishwa, tumedharirishwa sana,
Kama ni ku. . . . . . . .
Naweza kuendelea kuorodhesha mabaya yote na kujaza jamvi hili lakini niseme tu kwa ufupi kwamba yote hayo yamefanyika tukiwa chini ya chama cha mapinduzi tangu nchi yetu ipate uhuru. Hata hivyo, NURU YA MATUMAINI imeanza kuangaza na watanzania wengi tayari wameanza kusherehekea ushindi ambao muda si mrefu utapatikana. Ushindi huo si mwingine bali ni kukiangusha chama hiki kilichopoteza mwelekeo. Najua siku hiyo ipo na yaja tena i karibu sana.
Baada ya kukidondosha chama hicho, napendekeza chama tawala kipya kiiagize serikali yake itangaze siku mbili za mapumziko ili wananchi wapate muda wa kusherehekea ushindi au kwa lugha nyingine uhuru wa pili kwa taifa letu.
Naomba kuwasilisha.
Home »
» CCM Ikiangushwa Chama Tawala Kipya Kitangaze Siku ya Mapumziko Nchi Nzima


0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !