Headlines News :
Home » , » Patrice Lumumba (2 Julai 1925 – 17 Januari 1961) Jasiri Mzalendo zaidi kupata kutokea katika Ardhi ya Afrika

Patrice Lumumba (2 Julai 1925 – 17 Januari 1961) Jasiri Mzalendo zaidi kupata kutokea katika Ardhi ya Afrika

Written By Unknown on Wednesday 19 September 2012 | 09:31

Akiwa na miaka 34 alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, pia alikuwa ni kati ya viongozi wachache kabisa waliokuwa na “spirit” ya ki-Afrika na waliokuwa na upeo mkubwa na mategemeo ya kuwa na nchi ya Afrika yenye mafaniko makubwa pamoja na Kwame Nkrumah wa Ghana na Julius Nyerere wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwanaharakati wa Marekani aliyekuwa akitetea haki za watu weusi Malcolm X alipata kusema “Hakuna kiongozi jasiri na mwenye msimamo kupata kutembea katika Ardhi ya Afrika kama Patrice Lumumba”.

Mwanaharakati kutoka Amerika ya Kusini Ernesto Che Guevara alipata kusema “Kuuawa kwa Lumumba ni pigo kubwa kwani alikuwa nguzo imara na muhimu sana aliyekuwa anapingana kabisa mabepari waliokuwa wanyonyaji hivyo basi tuungane pamoja kuupinga kwa nguvu kabisa ubepari.



Soma historia na hotuba za kijasiri kabisa za Patrice Lumumba

Patrice Emery Lumumba



Alikuwa mwanasiasa na mwanamapinduzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mwaka 1958 alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa Chama cha Taifa cha Kongo (kwa Kifaransa:Mouvement National Congolais). Mwaka 1960 alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya kuongoza harakati za kupigania uhuru kutoka kwenye utawala wa kikoloni wa Wabelgiji. Baada ya miezi miwili tu ya kuwa Waziri Mkuu, Lumumba alipinduliwa na baadaye kutiwa ndani kabla ya kuuawa katika mazingira ya kutatanisha katika eneo la Katanga upande wa kusini wa Kongo.

Aliuawa kikatili sana baada ya mateso mengi ya kikatili aliyopewa baada ya kuonekana mwenye msimamo na asiyetaka kuruhusu namna yoyote ya unyonyaji na ukoloni mamboleo.



Mwaka 2002 serikali ya Ubelgiji iliomba msamaha kwa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kuhusika katika kifo cha Patrice Lumumba
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Followers

SEARCH THIS BLOG

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Habari Bongo - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template