Uvutaji wa sigara ni hatari sana kwa afya ya binadamu kwani sigara zaidi ya kemikali 4,000 ambazo mamia katika hizo ni sumu. Sigara husababisha madhara katika karibu kila sehemu ndani ya mwili na huweza kuharibu hata kinga mbalimbali za mwili wa binadamu.
Chembe za sumu za sigara husafiri ndani ya mwili na kusababisha matatizo kwa njia mbalimbali
(Nicotine) iliyoko ndani ya sigara hufika kwenye ubongo ndani ya sekunde kumi tu baaday ya mtu kuvuta ule moshi wa sigara. Huingia sehemu zote za mwili mpaka kwenye matiti .
(Carbon monoxide) (CO) ni sumu kali iliyoko kwenye sigara ambayo hujishika na (hemoglobin) kwenye chembe chembe hai nyekundu za damu na kusababisha seli zilizoathirika kushindwa kubeba oksijen ya kutosha.
(Carcinogens) inayopatikana katika moshi wa tumbaku husababisha kansa pia huua genes zinazo-regulate ukuaji wa seli na kusababisha seli hizo kukua taratibu sana au kwa haraka kupita kiasi.
Madhara yanayoletwa na uvutaji sigara
Written By Unknown on Wednesday, 19 September 2012 | 09:12
Labels:
mchanganyiko,
mpya
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !