Wakuu, wiki kadhaa zilizopita mtu moja alinipa mwongozo wa ccm kuhusu katiba mpya ulioandaliwa Dodoma na wajumbe waliotajwa hapo chini; Nimescan, kisha nikajaribu ku upload nimekwama, japokuwa nisingweza ku upload kurasa zote kwa kuwa una kurasa 27. Hata hivyo, nimewaandikia hoja mbili tu kati ya nyingi kwa ajili ya kuchokoza mjadala wakati ninaomba mwongozo wa jinsi ya ku upload kutoka kwa wataalam wa IT. Sijajua kama tatizo ni laptop yangu au kitu kingine. Ifahamike hoja mbili zilizoandikwa hapo chini nimecopy na kupaset. Sijabadilisha hata nukta wala koma.
NB; Kwa wale mlioangalia ITV waliporusha live kongamano la Katiba mpya yule mwanasheria wa ccm alizunguzia mwongozo wa ccm. Aliyasema yako humu kama alivyosema ila hakuzungumzia maeneo nyeti katibsa.
1)Mh.Andrew Chenge (MNC) (MB) -Mwenyekiti
2) Ndg Abdulrahaman O Kinana ( MNEC) Mjumbe
3)Mh Jenista Mhagama (MNEC) (MB) Mjumbe
4)Ndg Vuai Ali Vuai (MNEC) (MB) Mjumbe
5)Kingunge Ngumbalu Mwiru ( MNEC) Mjumbe
6)Machano Othaman ( MNEC) Mjumbe
7)Mh. Kidawa Hamid Saleh Mnec (MNEC) (MB) Mjumbe
8)Ndg Francis K. Mwonga Secretariet
9)Ndg Benedict E Lyamuya Secretariet – katibu
10)Ndg Salum Kh. Reja - Secretariet
HOJA Uchambuzi wa Chama
Tafakuri ya Chama.
E Utaratibu wa uteuzi wa Tume huru ya Uchaguzi i)Muundo wa Tume ya Uchaguzi kwa sasa unazingatia matakwa ya ibara ya 74 ya jamhuri ya Muungano, ambayo inatoa madaraka kwa Rais, kumteua mwenyekiti wa Tume na wajumbe wengine wanaotajwa katika sheria husika
ii) Wapo baadhi ya watu wanaohoji muundo huo na kudai kuwa, hauzingatii uwakilishi wa vyama vya siasa na kwamba wajumbe wake huteuliwa na Rais, ambaye pia ni kiongozi wa chama cha siasa kinachotawala. Kwa sababu hiyo, wajumbe wa Tume katika utendaji wao wa kazi ama watakuwa na upendeleo kwa chama husika au watakuwa wanalipa fadhila.
iii) Wenye hoja hii wanapendelea kuwe na ama uwakilishi wa vyama vya siasa au kuwe na Chomba kitakachochuja majina ya wajumbe wa Tume kabla ya Rais kuwateua. Kwa kuzingatia dhamana kubwa aliyonayo Rais wa Nchi kikatiba, ya kuwateua hata majaji, ni muhimu Rais akawateua pia wajumbe wa Tume ya Uchaguzi. Hata hivyo, ili kuimarisha uongozi wa Pamoja katika nchi yetu, sasa ni wakati muafaka wa kuanzisha utaratibu utakaoshirikisha Bunge katika uteuzi wa baadhi ya vyombo ya utendaji ikiwemo Tume huru ya Uchaguzi.
f Suala la Mgombea binafsi Yapo maoni ya baadhi ya watu kwamba, ipoa ha ya kuruhusu wagombea binafsi katika uchaguzi wa Urais, wabunge, Wawakililshi na madiwani bila kuwa wanachama au kupendekezwa na vyama vya siasa. Hoja yao ni kwamba, kutomruhusu kutomruhusu mgombea binafsi ni kumnyima haki yake ya kikatiba ya kushiriki katika shughuli za utawala wan chi na kuwanyima watu wengine haki ya kuchaguliwa ambao siyo wanachama wa chama cho chote cha siasa. Wananchi sio tu wanayo haki ya kuchagua viongozi wao kwa njia ya kidemokrasia bali vile vile wanastahili kufahamu na kupima itikadi , sera na dira ya wale wanaotaka kuwaongoza.
Aidha, Lengo la kuanzishwa vya kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa ni kushindanisha vyama na sio watu binafsi katika uchaguzi wa vyombo vya dola. Kuruhusu mgombea binafsi ni sawa na kuweka rehani uhuru na maendeleo ya wananchi na pia ni kudhoofisha nidhamu katika vyama vya siasa. Hata hivyo, endapo katika mjadala wananchi walio wengi watapendelea katiba iruhusu mgombea binafsi ni vyema yawekwe masharti maalumu ambayo mgombea binafsi ni lazima ayatimize.
CCM hawako tayari kuja katiba mpya kwa sababu;
Hawataki mgombea binafsi kwa kuweka masharti maalum kwa mgombea binafsi. Maalum ukiangalia wanalenga kuweka masharti magumu ambayo ni sawa na kukataa.
Pili, hakutakuwa na tume huru kwa wajumbe wake kuteuliwa na Rais na kupitishwa Wabunge ambao kimkakati inajulikana kuwa wengi wao ni wanaccm.
Hapa naanza kuamini kwamba katiba mpya inaweza kuwa Changa la Macho, It might be just my faithlessness.
Home »
mchanganyiko
,
mpya
,
siasa
» Mwongozo wa CCM kuhusu katiba mpya; Imefichuka wakwamisha Tume huru ya uchaguzi na mgombea binafsi
Mwongozo wa CCM kuhusu katiba mpya; Imefichuka wakwamisha Tume huru ya uchaguzi na mgombea binafsi
Written By Unknown on Monday, 17 September 2012 | 11:05
Labels:
mchanganyiko,
mpya,
siasa
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !