Headlines News :
Home » » Taarifa Kuhusu P- Square Kushtakiwa

Taarifa Kuhusu P- Square Kushtakiwa

Written By Unknown on Sunday, 9 September 2012 | 07:30

Unakumbuka ile kolabo ya P Square na Akon inaitwa Chop my money ambayo ilimfanya May D kuwa staa zaidi baada ya kuongezwa kuwa mtu wa nne kusikika kwenye hiyo single? kama hufahamu May D ni msanii wa Nigeria ambae alisainiwa kuwa chini ya lebo inayomilikiwa na P Square (Square Records) ambapo ni siku kadhaa zimepita toka lebo hiyo itangaze kwamba haimuhitaji tena na wala hayuko tena chini yao. Leo mtandao wa Naijag umeripoti kwamba May D ambae alitimuliwa na lebo hiyo wiki kadhaa zilizopita yuko kwenye hatua za mwisho za mazungumzo na wanasheria wake ili awashitaki P Square kwa kuvunja mkataba kiholela. May D anasema taarifa za kutimuliwa kwake alizipata kwenye blogs na magazeti kama walivyopata watu wengine na kwamba hakupewa taarifa zozote za kiofisi kama inavyopaswa, hiyo ndio sababu inayomfanya awashitaki P Square akiwemo kaka yao mkubwa Jude Okoye ambae ndio alitangaza kuuvunja mkataba wa May D.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Followers

SEARCH THIS BLOG

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Habari Bongo - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template