Itakumbukwa kuwa vyama vyote vya siasa hupata ruzuku kila mwezi kwa mujibu wa sheria. Ruzuku hizo zitatumika kuimarisha na kuendesha vyama hivyo kwa kadri itakavyoamuliwa na vyama vyenyewe. CCM kama vyama vingine imekuwa ikipata takriban 1.2billion hivi. Chama hiki kimekuwa kikitumia pamoja na mambo mengine kuwalipa mishahara viongozi wake wa kila Wilaya na mikoa lakini pia kulingana na kauli ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuwa pia Wakuu wa Wilaya na Mikoa wana ruhusa ya kuimarisha chama hicho popote walipo.
Ikumbukwe kuwa Mkuu wa Wilaya/Mkuu wa Mkoa analipwa posho na stahili zote yakiwemo magari ya kifahari kutoka kwenye bajeti iliyotengwa kuendeshea serikali. Pia huyu akistaafu atalipwa mafao kama mtendaji wa serikali. Kiongozi anapozungumza na kuachwa tu hivi ni kuwa tumeridhia kuwa CCM iwe na ruzuku ya zaidi ya 4.8billion kila mwezi (ukiongeza mishahara na marupurupu ya wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya) ukilinganisha na vyama vingine kama CHADEMA ambacho hupata wastani wa 233Million kwa mwezi na CUF 98Million.
My Take: Mara nyingi imegundulika kuwa Waziri Mkuu alilidanganya bunge kwenye majibu yake,Ni vyema sasa kupelekwa hoja binafsi kuhoji uhalali wa watendaji wa serikali kufanya kazi za CCM.
Ahsanteni.
Home »
» Hujuma: Budget ya Serikali inatumika kuimarisha CCM nchi nzima



0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !