Wana habari bongo, mwenendo wa kisiasa hapa nchini inajionyesha kabisa kwamba CHADEMA ni chama ambacho kitapata ushindi kwa asilimia kubwa. Japo kuwa wana CCM mta criticise lakini huu ndiyo mtizamo wa watu wengi sana kwa sasa ambao unapelekea kuwa kweli. Tizama tu mikutano ya CCM na CHADEMA, na ukisikia watu wengi wanavyoongea mitaani na vijijini ni kwamba Chama tawala kimezidiwa nguvu. Watu wengi wana jiuliza, je Chama tawala kitaweza kweli kukubali matokeo?, maana inavyoelekea watu wengi sana watakuwa wamepata mwenendo wa matokeo ya vituo vyote kupitia ripoti za mawakala wa vituo, na yatakuwa yanawekwa kwenye mitandao kila sekunde, kila dakika na hivyo kuona wazi kabisa chama kipi kinaongoza. Nahisi kutokea kama Zambia japo kuwa nchi haina watu wengi lakini waliyajuwa matokeo mapema mno ndani ya usiku huohuo na watu wakaingia mitaani kushangilia, vivyo hivyo hata sisi hapa Tanzania chaweza kutokea. Nahisi itakuwa vigumu kwa CCM kuamini kwamba kweli kimeshindwa, je kama hawataweza kuamini kitakachotokea, wana Jf itakuwaje, hebu tujaribu kupiga picha, mgombea wa Uraisi kutoka CCM ameshindwa, haiwezi kuwa kama ilivyotokea Kenya 2007 Kivuitu kutangaza Kibaki kashinda, na kuapishwa haraka haraka, au kama kule Ivory coast mpinzani aliyeshinda akakaa hoteli kwa ulinzi wa majeshi ya kimataifa huku Bagbo akidai mshindi na kuuda serikali. Na je vipi upande wa vyombo vyetu vya dola jeshi na polisi itakuwaje au wanaweza kupokea vipi matokeo hayo na kitu gani au hatua gani zinaweza kufuatwa. I have a dream: CHADEMA will win the 2015 election. Sure! this dream will come true. hofu ni kwamba upande mwingine i.e CCM na serikali kipindi hicho kabla ya kuapishwa itakuwaje?. sijui siku ya kuapishwa itakuwaje kwa hamasa ya watu na PEOPLES POWER!.
Home »
» Kuna kila dalili kwamba, matokeo ya uchaguzi 2015, raisi wa sasa aweza kukabidhi nchi CHADEMA



0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !