Home »
» Ujenzi wa daraja la kigamboni waanza
Ujenzi wa daraja la kigamboni waanza
Written By Unknown on Thursday, 13 September 2012 | 01:48
Ujenzi wa Daraja la Kigamboni umeanza
12/09/2012
Akisisitiza ubora wa kazi, Dkt. Magufuli alisema kuwa, Wizara yake ipo makini na kuwataka makandarasi kufanya kazi kwa usanifu mkubwa na wakichemka watawajibishwa kama ilivyokuwa kwa mkandarasi wa barabara ya Kilwa, “Nasema makandarasi wajue kuwa Tanzania si sehemu ya kujifunzia kazi, atakayefanya vibaya itamgharimu mwenyewe kwa kurudia ujenzi kwa gharama zake na hata kuchukuliwa hatua za kisheria. Kuanzia sasa, makandarasi watakaojenga chini ya kiwango watawajibishwa kwa kufukuzwa kazi mara moja na adhabu nyingine,” alisisitiza Magufuli.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli alikagua ujenzi wa daraja la Kigamboni akiwa ameambatana na viongozi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki, Mbunge wa Kigamboni Dkt.Faustine Ndugalile, jana jijini Dar es salaam. Daraja la Kigamboni linajengwa na kampuni ya China Railways Engineering kwa gharama ya shilingi bilioni 214 na linatarajia kukamilika kabla ya mwaka 2015
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !