Home »
» Yuko wapi rais Kikwete?wako wapi viongozi wa nchi?
Yuko wapi rais Kikwete?wako wapi viongozi wa nchi?
Written By Unknown on Sunday, 9 September 2012 | 14:17
Wadau naamini wote tunayajua mambo ya mauji ra raia wasio na hatia yanavyoendelea kiholela huku kukiwa hakuna nia ya dhati toka kwa viongozi wetu kuanzia wa serikali mpaka jeshi la polisi,bad enough kwa kua hao viongozi wanaouliwa sio ndugu zao,wanazidi kututia uchungu kwa kwa kutuona Watanzania ni mahayawani wa kutupwa kwa kuja na majibu ya kejeli na propaganda nyepesi juu ya mauaji yanayoendelezwa.
Kauli kama za Chagongja,Tendwa,Nape Nnauye na jana Wassira kupitia Tbc,ni kauli za dharau kwa Watanzania kwa vile wanatuchukulia ni mahayawani tusiokua na tafakari hata kidogo kwa mambo yaliyo na majibu ya wazi kama matukio hayo ya mauaji yanayoendelea!nimeangalia video ya tukio la vurugu za Iringa,video ambayo nina amini serikali na jeshi la polisi wasingependa ionekane kwa Watanzania kutokana na udhalimu waliofanya na uongo wa kitoto wanaojaribu kutupa Watanzania,katika video hiyo labda mwanadamu aliye na upeo wa level ya kuku ndie atakaekubaliana na matamko ya kipropaganda mfu yanayotolewa na viongozi wetu kama Wassira na Tendwa!!
Najiuliza kitu kimoja rais wetu Kikwete mbona yuko kimya hajatoa kauli hata moja kama vile mauaji haya ni halali kabisa!ni wazi kipindi cha mwalimu Nyerere mtu kama kamanda Kamuhanda na askari wote waliohusika na tukio lile kwa kua wameonekana wazi sasa hivi wangekua ndani ya mikono ya sheria!serikali yetu imeshndwa kutumia rasilimali zetu kuendeleza viwanda,kuendeleza elimu afya hata kulinda raia wenu mpaka mnabariki mauaji kwa sababu na propaganda zisizo na kichwa wala miguu.
Wakumbuke Mwi Nyerere alijenga viwanda,aliboresha elimu kwa kilimo tu,hakugusa madini wala kulangua ardhi kwa wageni,wao wanagawana madini,wanagawa ardhi kwa kisingizio cha uwekezaji kumbe ni uchukuaji,wameua viwanda,wanadidimiza elimu kiasi cha wasiojua kusoma na kuandika imeongezeka (wanatengeza taifa la wajinga) bado hawaridhiki na sasa wameamua kuua raia wake bila hatia!ila wakumbuke kua bila kuchukua taadhari ukweli ni kua mwisho wa yote uko mlangoni,dalili za raia kuto ogopa wala kuheshimu vyombo vya dola hasa polisi,maandamano ya juzi ya waislamu yenye sauti kali mpaka waziri kusalimu amri,ni wazi sasa Watanzania hawako tayari kuendelea kunyanyaswa na wanajua haki zao zinakandamizwa na wachache!viongozi amkeni sasa kabla ya kuchelewa
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !